KWANGU HUNA MWENZA
1. Moyo hausemezeki, na akili
iko pweke
Mwengine hanimiliki, yeye
kipenzi peke
Milele simbanduki, nataka
mahaba yake
Tuwaache wenye chuki, penzi sitetereke.
2. Nianze wapi kukusifu, angalau
usifike
Umbile la Ashrafu, sina
budi nitamke
Ametukuka Latwifu, kakupamba
mja wake
Na kukupa maelfu, ya
vipaji vitumike.
3. Umepewa maelfu, ya uzuri
utumike
Kwenye yalo maarufu, yasifiwayo kwa mke
Kwako wewe nimekifu, kusudi nisisumbuke
Uninukishe harufu, na
wardi lichanuke
4. Toka juu hadi chini,
inapasa usifike
Nywele ndefu na laini, na
macho yenye upeke
Tabasamu mdomoni, uzuri
wa umbo lake
Ahsante na shukrani,
mevifanya wimbo wake.
5. Uwe ni kama barafu,
mtima wangu shwarike
Na kwa moyo mkunjufu, pendo lako nifunike
Niipate tahafifu, na maradhi yaponyeke
Nakupenda maradufu, sauti yangu sikike
kweli chawakama-suza mumeamua mwaka huu hongereni
JibuFuta