TUZIENZI MILA ZETU
1.
Bismilahi
Azizi, nataka kuelezeni
Nizidishie na pumzi, niwaeleze
wandani
Bila kuwa pingamizi, nioneshe
ya moyoni
Bustani tuenzi, izidishe
kushaini
2.
Nieleze
waziwazi, vijana wa visiwani
Utamaduni tuenzi, na
asili ya zamani
Vizazi tuviaidhi, wasivamie
mageni
Bustani ndio enzi, kwetu
sisi wezanguni
3.
Tujuwe
mavazi yetu, mababu waloshaini
Hawakukubali katu, wigi
modo kusheheni
Kanzu mavazi yetu, kwa nini
hamutakani
Utamaduni ni wetu, mzaha
tuuwachie.
4.
Si
kanga si mrekani, hata lugha namba wani
Mwambao ndio makini, vilugha vi mitaani
Kizungu ni lugha gani, nawauliza
makwini
Utamaduni ni wetu, mzaha
tuuwacheni.
5.
Naacha
kalamu yangu, nadhani nakuchosheni
Ikiwa wazimu wangu, mutanijadili
ndani
Au nawakumbusheni, muuachie
ugeni
Mila zetu turudie, tusivamie
mjini.
Bishara Mohamed Ali-SUZA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni