LUGHA
1
Ni roho ya walimwengu, maulama na mazuzu
Si kwa hao wazungu, hata wavao kanzu
Sio kwa uwezo wangu, bali mwenyewe aghazzu
Anaye haribu lugha, mwerevu au mjinga?
2
Awali ya kwa wazawa, huisanifu kinamzu
Na tena kwa kuijua, kwa mizani nayo vinazu
Ni vipaji wamwpewa, vya
namna kwa agazzu
Anayeharibu lugha, mwerevu au mjinga?
3.
Hupelekwa na shuleni, jinsia na kanzu
Bila ya kumughini, na tena kwa kumghizu
Sio tu kwa masikini, hata tajiri wa enzu
Anayeharibu lugha, mwerevu au mjinga?
4
Husoma na kubobea, tafauti za fanizu
Pia yao historia, kwa madaha na kughazu
Na hata sayansia, walimu na marubani
Anayeharibu lugha, mwerevu au mjingi
5
Ila watungapo chuo, mambo yote tafarani
Huona ja ufunuo, utokao kwa manani
Kila wao mkupuo, lugha mbili zihewani
Anayeharibu lugha, mwerevu au mjinga?
6.
Kila ya moja wapo, mkorogo
hutawala
Mbali mbali zawapo, mbili lugha mikabala
Huhisi elimu ipo, kichwani yawatawala
Anaeharibu lugha, mwerevu au mjinga?
7
Huonwa wasomana, wawanaoitumia moja
Muda si wa kwao tena, wala
hawaleti tija
Hujihisi kwa maana, wanazuoni wareja
Anaeharibu lugha, mwerevu au mjinga?
8
Wanazuoni wa sasa, hilo kwao muamko
Maendeleo ya sasa, na vingi vyao vituko
Mkorogo wa kisasa, kwa nderemo na vichekeso
Anaeharibu lugha, mwerevu au mjinga?
MTUNZI: SULEIMAN SALIM SULEIMAN
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni