BAHARI IMECHAFUKA
Bahari imechafuka, samaki wakimbizana
Na hali ikachafuka , kuona wakipishana
Buhuri ikasikika , kama kwamba ni mchana
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani.
Wakubwa waliwacheka , wadogo zao kwa
sana
Kuona wadhalilika , kukosa yao hiyana
Wengi wao kukereka , kuonewa na
mabwana
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani
Furaha yao kufika , katika kila kona
Ingawa si ya mipaka, lakini
yatakikana
Itakuwa patashika , kelele kila namna
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani
Maji haya yazunguka , kwa wimbi
lisonekana
Samaki mekushanyika , wamejazajazana
Mawimbi yanasikika , watu kazi kunong´ona
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani
Haya twende kwa haraka , samaki
wakimbizana
Ni yetu hiyo sadaka , wakubwa
watakikana
Muafaka kuweka , tusije hitalifiana
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani
Ndani ya hili shitaka , musije
mukatuona
Ndimi zetu ni mashaka , kwa
tunayoambizana
Ndo mimi na huyu kaka , tulivyokwisha
nong'ona
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa jamani
Tangu kale hadi leo , hatujaona
lamana
Tena kwa ukali wao ,eti wanafokeana
Toeni zote komeo , tunataka kupambana
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani
Ajira sasa haziko , wapi zapatikana
Tunataka mabadiliko , hebu tizameni
sana
Kutwa ni mahangaiko , usiku tunakabana
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani
Kama nyinyi hamuwezi , sisi
tunatakikana
Kudai yetu agizi , kwa wanaotubana
Tunataka mageuzi , wazee pia vijana
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani
Vijana tuunganeni , kudai yetu hiyana
Ili tuishi duniani , bila ya
kuoneyana
Wakubwa wamapangoni , wameridhika na
ubwana
Wanaruka kwa hasira , samaki hawa
jamani.
SAADA MABROUK JUMA- CHAWAKAMA SUZA
SAADA MABROUK JUMA- CHAWAKAMA SUZA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni